SIASA IONDOLEWE KWENYE MIKATABA
Na Elias Mhegera Mjadala mkubwa unaoendelea nchini Tanzania kwa sasa ni kuhusu yaliyojiri kuhusiana na ‘mchanga’ wa dhahabu au ‘makinikia’ na pia athari zake baadaye kisiasa na kisheria pia. Watanzania wamechachamaa kwa hamasa kubwa, wakiwashambulia wabunge wao kwa kuruhusu mambo ya aina hii yaendelee kwa muda mrefu kwa sababu za kulindana na kutumia wingi wa wale waliokuwa wanaunga mkono. Wadau mbali mbali wanapendekeza kwamba mikataba yote ya madini ijadiliwe upya. Lakini pia wanataka sheria za mikataba zizingatiwe ili taifa ingie matatani na wawekezaji Wananchi kwa ujumla wanaona kwamba kuna miswaada ilipitishwa kwa hati ya dharura ka malengo mabaya. Na haya yote yaliwezekana kwa sababu ya mfumo mbovu wa kisiasa. Mjadala wa jambo hili ni mpana ipo ya kisheria, na kisiasa pia. Prof. Abdallah Safari ambaye ni wakili wa kujitegemea pamoja na kwamba yeye pia ni makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) anasema hili ni janga jingine. Anaiona hofu kwamba uam...