Asilimia 70 ya vijana hawana ajira

Na Mwandishi Wetu

VIJANA saba kati ya kumi kwenye nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara ikiwemo Tanzania wamebainika kuwa hawana ajira.

Hali hii inaufanya ukanda huu kuwa wa kwanza kwa kuwa na idadi kubwa ya vijana wasio na ajira na ndio ukanda wenye vijana maskini kuliko kanda zote barani Afrika na duniani.

Ripoti ya mapitio ya ukosefu wa ajira ya mwaka 2016 iliyotolewa Agost 24 mwaka huu na Shirika la Kazi Duniani (ILO) imeonyesha kwamba hili ni punguzo la asilimia 10 katika kipindi cha miaka 15 iliyopita.

“Hii inabainisha kwamba idadi ya vijana wenye umaskini wa ajira kwenye ukanda huu imeongezeka kwa asilimia 80 katika kipindi hicho cha miaka 15 iliyopita,” ilisema taarifa hiyo ambayo Raia Mwema ina nakala yake.

Kwa mujibu wa tafsiri mbalimbali, kijana ni mtu yeyote mwenye miaka kuanzia 18 na kuendelea, japokuwa kwa mujibu wa sheria za kazi zinamtambua kijana ni yule mwenye umri wa miaka kuanzia 15 mpaka 35.

Kuongezeka kwa idadi ya vijana walioko kwenye umaskini wa kutupwa ni kupungua kwa ukuaji wa uchumi miongoni mwa nchi zinazoendelea zilizoko kwenye ukanda huu.

Ripoti hiyo imebainisha kwamba kwa upande wa Afrika Kaskazini vijana wanne kati ya kumi wanakabiliwa na umaskini wa kutupwa au umaskini wa ajira.

Katika kipindi cha miaka 15 iliyopita, umaskini wa ajira kwa vijana umepungua kwa asilimia zaidi ya 50.

Hata hivyo, ripoti hiyo imebainisha kwamba kuanzia mwaka 2012, hakukuwa na dalili zote za kupunguza idadi ya vijana maskini kwenye ukanda huo, na umaskini kwa watu wazima nao bado sio mkubwa kama wa Kusini mwa jangwa la Sahara.

Kwa upande wan chi za kiarabu, asilimia 39 ya vijana wanaofanya kazi wanaishi kwa kipato cha chini ya dola za Marekani 3.10 kwa siku ikilinganishwa na watu wazima asilimia 35 wanaishi kwa kipato hichohicho.

Ripoti hiyo imeonyesha kwamba idadi ya vijana maskini walioko kwenye ajira imeongezeka kwa asilimia tatu kuanzia mwaka 2007 lakini hakukuwa na mabadiliko kwa idadi ya watu wazima wasio vijana.

Kwa upande wa ukanda wa Asia Mashariki, idadi ya vijana maskini wenye ajira inaendelea kushuka kwa kasi na kufikia asilimia 13.8 mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Asia Kusini ndiyo inafuatia Kusini mwa jangwa la Sahara kwa kuwa na idadi kubwa ya vijana maskini wenye ajira kwani ni asilimia 50, yaani nusu ya vijana wote.

Hata hivyo, ripoti hiyo imeonyesha kwamba kumekuwepo na maendeleo makubwa ya kupunguza maskini vijana kwenye ukanda huo tokea mwaka 2007 ambapo idadi ilikuwa asilimia 70 kama ilivyo Afrika ya Kusini mwa jangwa la Sahara.

Imebainishwa kuwa, idadi ya vijana maskini itaendelea kushuka katika ukanda huo wa Asia Kusini kwa miaka michache ijayo.

Lakini, japokuwa idadi hiyo inapungua, idadi ya watu wazima wenye umaskini wa ajira ndiyo ilipungua sana kwenye ukanda huu katika kipindi hicho ikilinganishwa na kundi la vijana.

Katika ukanda wa Latino na Caribbean, idadi ya vijana waishio kwenye umaskini wa ajira ni kidogo sana na kuuufanya ukanda huu kuwa wa pili kwa idadi ndigo ya maskini vijana.

Imeelezwa kwamba kuanzia mwaka 1991, ukanda huu umefanikiwa kupambana na tatizo ya umaskini wa ajira kwa vijana kwa zaidi ya asilimia 50 na kuondoa pengo lililopo kati ya maskini vijana na watu wazima maskini.

Mwisho

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Tanzania inflation jump to 6.4 pc

DSE all share index down

Kibo inches closer to completion of gold assets sale to Opera